Monday, July 20, 2020

Mgombea Ahaidi Kuweka Pazia Mlima Kilimanjaro

ImageKada wa chama cha Mapinduzi (CCM) anayeimba kuteuliwa na chama hicho kuteuliwa kugombea ubunge kwenye jimbo la Moshi Mjini Omary Mwariko amehaidi kuweka pazia kwenye mlima Kilimanajaro iwapo atachaguliwa kushika nyadhifa hiyo.

Akizungumza leo wakati wa kuomba kura kwa wajumbe wa chama hicho kwenye ngazi ya Wilaya mjini Moshi wakati wa zoezi la upigaji kura wilayani humo.

“Ninachoomba mkinipa kura mtaona mambo ambayo hajawahi kuona hapa hata mlima Kilimanjaro huu nitaweka pazia hapa Moshi nataka pawe mji mtakatifu pawe sehemu patakatifu kuliko miji yote hapa nchini” amesema.

Ikumbukwe kuwa mchakato wa awali wa kuchagu wagombea wa uchaguzi ujao ndani ya chama umeanza rasmi leo Julai 20,2020.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/07/20/mgombea-ahaidi-kuweka-pazia-mlima-kilimanjaro/

No comments:

Post a Comment