Tuesday, July 21, 2020

Makonda: Nimepata pole nyingi kutokana na matokeo ya jana

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema amepokea pole nyingi katika matokeo ya jana ya kura za maoni katika jimbo la Kigamboni.

Makonda amesema jambo la kwanza anawashukuru kwa upendo wenu na maombi ya kumtakia mafanikio katika kutimiza ndoto yake.

“Jambo moja kubwa na muhimu ni kuyajua mapenzi ya Mungu na katika hili mapenzi ya Mungu ni makubwa kuliko mapenzi yangu,” aliandika ujumbe huo katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii.

Aliongezea kuwa “Nawatakia baraka na afya njema siku zote za maisha yenu asanteni sana sana wana Kigamboni kwa upendo wenu na kulipa nafasi niwe sehemu ya maisha yenu,”.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/21/makonda-nimepata-pole-nyingi-kutokana-na-matokeo-ya-jana/

No comments:

Post a Comment