Friday, July 17, 2020

Kisa cha Hospitali Iliyowalahai Wananchi TSh 814 Milioni kwa Vipimo Feki vya Covid19

Coronavirus: Healthcare facility proprietor arrested trying to ...

Mohammed Shahed alikamatwa na polisi alipokuwa akitorokea nchi jirani ya India. Picha: Hisani.

Janga la virusi vya corona si geni tena, si humu Tanzania tu bali ulimwenguni kote. Virusi vya corona vimesababisha mahangaiko makubwa kwa mataifa, watafiti wakikesha na kushinda muda wote kutafuta suluhu.

Lakini je umewahi kufikiri kuwa kuna baadhi ya watu ambao wanasherehekea  kuwepo janga la corona?

Mmiliki wa hospitali moja nchini Bangladesh amekamatwa na kuzuiliwa na maafisa wa polisi baada ya kubainika kuwa hospital yake imewalaghai wananchi zaidi ya $350,000 (TSh 814,000,000 kwa kuwafanyia vipimo na matokeo feki ya covid19.

Msemaji wa Serikali ameeleza kuwa Mohammed Shahed alikamatwa na polisi alipokuwa akitorokea nchi jirani ya India baada ya kuwa mafichoni kwa muda.

Bangladeshi hospital owner arrested over fake virus tests - Los ...

Polisi sasa wamepewa idhini kumzuilia Shahed kwa siku 10 zaidi. Picha: Hisani.

Shahed anadaiwa kufanya vipimo hivyo vya covid19 kwa malipo licha ya serikali kutangaza kuwa vipimo hivyo vifanywe bure, kando na hivyo matokeo yake ni feki.

Kwa mujibu wa msemaji wa serikali, hospitali hiyo imefanya vipimo na kutoa zaidi ya matokeo 6500 feki huku 4000 zikiwa za kufaa.

Kando na hivyo, hospitali hiyo inadaiwa kutoa vyeti vya corona kwa malipo hata bila kufanyka vipimo.

Kwa, mujibu wa CNN, maafisa wa polisi sasa wamepewa idhini kumzuilia Shahed kwa siku 10 zaidi huku uchuguzi kuhusu kisa hicho kikiendelea.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/17/kisa-cha-hospitali-iliyowalahai-wananchi-tsh-814-milioni-kwa-vipimo-feki-vya-covid19/

No comments:

Post a Comment