Friday, July 17, 2020

Jamaa Aichoma Nyumba Yake Usiku Baada ya Kubugia Pombe

Detroit Fire Department photo: 'Insensitive' picture of ...

Waliamka asubuhi na kupata nyumba ya mlevi huyo imechomeka. Picha: Hisani

Bwana huyu alirudi nyumbani akiwa amelewa na kuanza kubomoa nyumba ya mpangaji katika ploti ya babake

Majirani wenye mori walibomoa jikoni yake kama njia ya kisasi

Waliamka asubuhi na kupata nyumba ya mlevi huyo imechomeka

Pombe ni kinywaji ambacho huweza kuleta raha na vile vile karaha kulingana na jinsi mnywaji anavyopenda kukitumia.

Bwana mmoja amewaacha wengi vinywa wazi katika kaunti ya Meru baada ya kubainika kuwa aliiteketeza nyumba yake baada ya kurudi nyumbani usiku akiwa amelewa chakari.

Kulingana na kisa hicho kilichopeperushwa katika runinga ya NTV, bwana huyo alirudi nyubani usiku na kuanza kulimomoa  dirisha la nyumba ya mpangaji kwenye ploti ya babake.

Licha ya majirani hao kujaribu kumzuia asimharibie mpangaji huyo makazi, aliendelea akisema kuwa mali hiyo ni babake na kuwa ana haki ya kutenda atakalo kwayo.

Royalty-Free photo: Photo of burning house | PickPik

Haijabainika ni kwanini jamaa huyo aliamua kutekeleza kitendo hicho. Picha: Hisani.

‘Majirani walimwambia kuwa wangeharibu jikoni yake kama njia ya kisasi maana alivunja dirisha la mpangaji,’’ mmoja alisema.

Baada ya majirani hao wenye mori kuibomoa jikoni yake, walienda kulala huku wakimuacha jamaa akipiga makeke.

‘’ Tulimuacha akipiga kelele lakini tulipoamka asubuhi, tulipata ameichoma nyumba yake, mwengine alisema.

Haijabainika ni kwanini jamaa huyo aliamua kutekeleza kitendo hicho.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/17/jamaa-aichoma-nyumba-yake-usiku-baada-ya-kubugia-pombe/

No comments:

Post a Comment