Friday, July 10, 2020

Dondoo za leo;Dk. Mwinyi : Kupata ushindi Zanzibar ni mgumu, Mwili wake wapatikana, Wasema hawatishiki naye

Habari ya asubuhi mdau wa Opera News, tunatumai u bukheri wa afya.

Karibu katika dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari nchini asubuhi ya leo.

Zinazobamba ni pamoja na kupata ushindi Zanzibar mgumu asema Hussein, Mwili wa mama aliyewatupa wanawe mtoni wapatikana na mwisho ni juu ya ACT kudai kuwa hawatishiki na Dk. Mwinyi. Karibu;

HUSSEIN: KUPATA USHINDI ZANZIBAR NI MGUMU

KAZI ya kuutafuta ushindi kwenye uchaguzi mkuu visiwani Zanzibar ni ngumu.

Hiyo ni kauli ya Dk. Hussein Mwinyi, mgombea urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), aliyoitoa baada ya kuchaguliwa na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho leo tarehe 10 Julai 2020.

Kwenye uchaguzi huo, Dk. Mwinyi amechaguliwa kwa kura 129 (asilimia 78.65), Shamsi Vuai Nahodha akipata kura 16 (asilimia 9.76) na Dk. Khalid Salum Muhamed akipata kura 19 (asilimia 11.58).

Soma zaidi>>>

MWILI WAKE WAPATIKANA

Miili ya watoto wawili na mama yao ambaye inaaminika aliwatupa ndani ya mto Nzoia Jumapili, Julai 5 kabla ya kajitupa imepatikana.

Winny Kulangwa mwenye umri wa miaka 24 anashukiwa kuwatupa wanawe watatu wenye umri wa mwaka mmoja na miaka minne majira ya saa tatu usiku.

Mwanawe mwenye umri wa miaka saba hata hivyo aliponea tukio hilo kwa tundu la sindano.

Familia ya Kulangwa ilisema kuwa marehemu hakuonesha matatizo yoyote ya kuzongwa na mawazo kabla ya kutenda kisa hicho.

Soma zaidi>>>

WASEMA HAWATISHIKI

CHAMA cha ACT-Wazalendo kimejipanga vyema kuibuka na ushindi wa kishindo katika nafasi ya Urais visiwani Zanzibar na kwamba hakibabaishwi na mgombea wa Chama cha Mapinduzi aliyepitishwa na halmashauri kuu ya chama hicho Jijini Dodoma leo,Dkt Hussein Mwinyi.

Akizungumza na The Guardian Digital muda mfupi tu baada ya kupitishwa kwa mgombea wa CCM, Katibu Mkuu wa chama hicho, Ado Shaibu ametamba kuwa mgombea waliyemuandaa hawezi kushindwa uchaguzi huo kwa kile alichodai kuwa ana uzoefu wa kutosha katika siasa za Zanzibar.

Soma zaidi>>>



source http://www.bongoleo.com/2020/07/11/dondoo-za-leodk-mwinyi-kupata-ushindi-zanzibar-ni-mgumu-mwili-wake-wapatikana-wasema-hawatishiki-naye/

No comments:

Post a Comment