Wednesday, July 15, 2020

Dereva wa basi asababisha ajali makusudi, awaua abiria 21 kulipiza kisasi

Deliberate accident: Bus driver crashes vehicle killing 21 people over demolition of his house

Awali alipewa fidia ya $10,360 kabla ya kubomolewa nyumba yake,ofa ambayo alikataa kupokea. Picha: Hisani

Kisa hicho kilifanyika mjini Anshun mkoa wa Guizhou Uchina

Kwa mujibu wa polisi, Zhang ambaye alikuwa dereva wa basi hilo alifariki pamoja na wanafunzi wengine 21

Dereva huyo alisababisha ajali kulipiza kisasi baada ya nyumba alimokuwa akiishi kubomolewa.

Dereva mmoja wa basi amesababisha ajali makusudi na kuwaua watu 21 na kuwajeruhi wengine 15 kama njia ya kulipisa kisasi.

Kisa hicho kilifanyika katika mji wa Anshun mkoa wa Guizhou Uchina, dereva huyo akisemekana kuchukua hatua hiyo kufuatia kubomolewa kwa nyumba alimokuwa akiishi.

Kulingana na taarifa ya polisi, Zhang ambaye alikuwa dereza wa basi hilo ni kati ya watu 21 moja walioangamia katika ajali hiyo pamoja na wanafunzi wengine 12 waliokuwa wakitarajia mtihani wao.

‘’Zhang alihuzunishwa na maisha yake haswa baada ya nyumba yake kubomolewa. Ili kujulikana mahangaiko yake, aliamua kufanya makosa makuu,’’ CNN iliripoti.

Kwa mujibu wa ripotiya CNN, Zhang alipaswa kuingia zamu mwendo wa adhuhuru lakini siku hiyo akaamua kuingia asubuhi akishika zamu ya dereva mwenza.

Alifanya hivyo baada ya kufika nyumbani asubuhi na kupata nyumba yake imebomolewa, hivyo akakimbia kazini kulipiza kisasi baada ya kukosa pa kuingia.

Awali alipewa fidia ya $10,360 kabla ya kubomolewa nyumba yake,ofa ambayo alikataa kupokea.

Deliberate accident: Bus driver crashes vehicle killing 21 people over demolition of his house

Inadaiwa kuwa baada ya kugundua kuwa nyumba yake ilibomolewa, alinunua kileo kikali kabla kuingia kazini akiwa na hasira.

Kabla ya ajali hiyo, alituma ujumbe kwa mpenziwe akieleza kuhusu jinsi alivyojawa hasira.

Nyumba ya Zhang ilibomolewa kutoa nafasi ya upanuzi wa barabara.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/15/dereva-wa-basi-asababisha-ajali-makusudi-awaua-abiria-21-kulipiza-kisasi/

No comments:

Post a Comment