Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, leo anatarajia kukabidhi ofisi kwa Mkuu wa mkoa huo Aboubakar Kunenge.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa imeeleza kuwa Makonda atafanya makabidhiano hayo ya ofisi majira ya saa 7 mchana jijini Dar es Salaam.
Julai 15, 2020 Rais John Magufuli alifanya uteuzi wa viongozi wa mikoa na wilaya na kumteua Abubakar Kunenge kuwa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam.
Kabla ya uteuzi huo Kunenga alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam na kuteuliwa kuchukua nafasi ya Paul Makonda.
source http://www.bongoleo.com/2020/08/01/makonda-kukabidhi-ofisi-leo-kwa-mkuu-wa-mkoa-wa-dar-es-salaam/
No comments:
Post a Comment