Friday, July 17, 2020

Rais Magufuli amefanya uteuzi mwingine awatumbua wakuu wa Wilaya akiwemo Sophia Mjema

Rais John Magufuli amefanya uteuzi mwingine leo na kuwateua viongozi mbalimbali.

Rais Magufuli amemteua Dk. Seif Shekilage kuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Songwe.

Kabla ya uteuzi huo Dk. Shekilage alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu na anachukua nafasi ya David Kafulila.

Rais Magufuli amemteua Mussa Ramadhani Chogelo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala mkoani Dar es Salaam.

Kabla ya uteuzi huo Chogelo alikuwa Ofisi ya Rais na anachukua nafasi ya Sophia Mjema.

Aidha, Magufuli amemteua Aswege Kaminyonge kuwa mkuu wa Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu.

Kabla ya uteuzi huo Kaminyonge alikuwa Ofisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya na anachukua nafasi ya Dk. Seif Shekilage ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Songwe.

Rais Magufuli amemteua Calorius Misungwi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa.

Kabla ya uteuzi huo Misungwi  alikuwa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na anachukua nafasi ya Julieth Binyura.

 

 



source http://www.bongoleo.com/2020/07/17/rais-magufuli-amefanya-uteuzi-mwingine-awatumbua-wakuu-wa-wilaya-akiwemo-sophia-mjema/

No comments:

Post a Comment