
Chelsea inatazamia kuchanga hela kumsaini Kai Havert. Picha;Hisani
Ng’olo Kante huenda akaigura Chelsea hivi karibuni na kujiunga na Real Madrid
Kante alihamia Stamford Bridge 2016 baada ya kuisadia Leicester kujinyakulia ushindi wa ligi ya premia kwa mara ya kwanza kabisa
Mkuu wa klabu ya Chelsea Frank Lampard hadi sasa ni wazi kuwa amemaliza mipango ya kumruhusu N’golo Kante kujiunga na klabu ya Real Madrid kama njia ya kuchanga hela tayari kumsaini Kai Havetz.
Klabu hiyo tayari imekamilisha dili ya kumsaini Hakim Ziyech wa Ajax pamoja na Timo Werner wa RB Leipzig shughuli iliyogharimu £85.
Kando na hivyo, iwapo Chelsea itahitaji kuwasaini wachezaji zaidi, italazimika kuwauza wachezaji wengine kufunga dili.
Kwa mujibu wa jarida la SunSport, nyota wa Bayer Leverkusen yuko tayari kuihama klabu yake, Stamford Bridge ikiwa mbioni kumnyakua.
Kanté. A man who gets way too much disrespect on here.
– 8th in the Ballon d’Or
– Premier League Player of the Year
– Premier League Champion with two different clubs
– World Cup winnerOne of the best midfielders of his generation. pic.twitter.com/bvqK6Xv1yd
— LDN (@LDNFootbalI) July 10, 2020
Chelsea italazimika kufikia gharama ya £90 milioni kabla ya klabu yake kumruhusu kuondoka.
Nyota huyo wa Ufaransa ni mmoja wa wachezaji ambao wameweza kushinda ligi ya premia akichezea klabu mbili tofauti mtawalia na hata kuibuka mchezaji bora wa msimu.
Kante ameonyesha ugwiji si kwa kuchezea kiungo cha ulinzi tu bali pia kati.
source http://www.bongoleo.com/2020/07/13/chelsea-yataja-mchezaji-wanaotarajia-kumuuza-ili-kumsaini-nyota-wa-ujerumani/

No comments:
Post a Comment