KIONGOZI wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amemteua aliyekuwa Waziri wa Mmabo ya Nje, Bernad Membe, kuwa mshauri Mkuu wa chama.
Zitto ametumia mamlaka ya Katiba ya ACT -Wazalendo kifungu cha 83 (1) (d) ambacho kinampa mamlaka ya kuteua washauri wa chama.
Wakati huo huo, Zitto amemteua Emmanuel Mvula ambaye ni wakili kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu.
Wote wamethibitishwa na Halmashauri Kuu ya chama inayoendelea na vikao vyake leo Agosti 3, 2020.
Aidha ACT-Wazalendo inaendelea na vikao vyake vya Hamshauri Kuu ya Taifa kuelekea mkutano Mkuu Augusti 5 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
source http://www.bongoleo.com/2020/08/03/zitto-amemteua-membe-kuwa-mshauri-mkuu-wa-chama-cha-act-wazalendo/
No comments:
Post a Comment