Monday, August 3, 2020

Serikali ya Magufuli Yachukua Hatua Kali Dhidi ya Wanaosambaza Habari za COVID19 Mitandaoni

After getting pregnant, you are done': no more school for ...

Magufuli amemshukuru Mungu kwa kuiponya Tanzania na kuikinga dhisi ya Covid19. Picha: Hisani

Mamlaka ya habari na mawasiliano imetoa nambari maalum kwa wananchi ili kuwaripoti watakaotoa habari feki kuhusiana na covid19

Rais Pombe Magufuli amesisitiza kuwa Mungu ameiokoa Tanzania kwa kuiondolea virusi vya corona

Tanzania ilikoma kutangaza habari zozote kuhusu covid19 Aprili, 2020

Serikali ya Tanzania imechukua mkondo mwingine katika kupambana na virusi vya corona pamoja na woga unaombatana nao.

Mamlaka ya habari na mawasiliano TCRA imetoa taarifa ikiwaomba wananchi  kumripoti mtu yeyote anayesambaza habari feki kuhusu virusi hivyo hatari mitandaoni.

Katika taarifa, TCRA ilitoa nambari ya simu maalum ambako habari zozote za kupotosha kuhusu virusi hivyo vitaripotiwa ili kuchukuliwa hatua wanaozichapisha.

Kwa mujibu wa mamlaka hiyo, habari hizo za kuchochea katika makundi mbali mbali za whatsap na Facebook ama katika mitandao yoyote ya kijamii zitaripotiwa katika nambari hiyo maalum.

‘’Ukipokea au ukiona ujumbe unaochochea, Kuzusha au kupotosha taarifa za corona katika group lako au lolote lingine mtandaoni, piga picha ujumbe huo na namba ya aliyeituma na utumie kwa TCRA kupitia namba 0737 300 300 au barua pepe: nocorona@tcra.go.tz’’ taarifa hiyo

Tanzania urges citizens to report individuals spreading fake COVID-19 news on social media

Hatu hii inajiri siku chache baada ya waangalizi mbali mbali kuishutumu serikali ya Magufuli kwa kukosa kutoa habari kamili kuhusu maambukizi ya virusi hivyo.

Serikali ya Tanzania ilisitisha shughuli ya kutoa taarifa za covid19 Aprili 2020, taarifa ya mwisho iliyotolewa na wizara ya afya ikibainisha kuhusu visa 509 vya maambukizi, vifo 21 na 183 waliopona.

Tanzania urges citizens to report individuals spreading fake COVID-19 news on social media

Tanzania ilikoma kutangaza habari zozote kuhusu covid19 Aprili, 2020. Picha: Hisani

Katika visa viwili tofauti, Rais Magufuli ametangaza kuwa nchi yake haina virusi vya corona tena na kuwa wagonjwa wote waliweza kupona.

Rais Magufuli ameiongoza Tanzania katika kumshuru Mungu kwa kuikinga na kuiponya nchi yake kutokana na virusi hatari vya corona.



source http://www.bongoleo.com/2020/08/03/serikali-ya-magufuli-yachukua-hatua-kali-dhidi-ya-wanaosambaza-habari-za-covid19-mitandaoni/

No comments:

Post a Comment