Safari za ndani kwa ndani zilifunguliwa Julai 25. Picha: Hisani
Safari za ndege zilipigwa marufuku kwa miezi minne
Waziri mkuu alitangaza Alhamisi, Julai 30 kuhusu kufungua anga tena Jumatatu, Agosti 5
Wasafiri watahitaji cheti za COVID19 ili kusafiri
Safari za ndani kwa ndani zilifunguliwa Julai 25
Nchi ya Somalia imefuata Kenya katika kufungua anga kwa safari za ndege za kimataifa miezi minne baada kuifungua kufuatia mlipuko wa virusi vya corona.
Safari hizo za kimataiga zimeanza rasmi Jumatatu, Agosti 3 chini ya masharti makali.
Safari za ndege zilipigwa marufuku kwa miezi minne baada ya kulipuka covid19. Picha:Hisani
Kwa mujibu wa taarifa ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo Maareye, wasafiri wote watakaoabiri ndege ama kutua nchini humo watahitaji kumiliki cheti cha kubainisha hali yao kuhusiana na virusi vya corona. Vyetu vikitakiwa viwe vimetolewa chini ya saa 72 kabla ya kusafiri.
Somalia iliweza kufungua safari za ndege za ndani kwa ndani Juali 25 huku ikitangaza masharti makali kuhusiana na safari hizo.
Kando na safari za ndege, kiongozi huyo alitangaza kuwa shule na taasisi zote za elimu kijumla zitafunguliwa Agosti 15, 2020.
Nchi hiyo ilipiga marufuku shughuli kadhaa ikiwemo za mawanda kama njia ya kuzuia maambukizi zaidi ya virusi vya corona.
source http://www.bongoleo.com/2020/08/03/covid19-somalia-yafungua-safari-za-ndege-kimataifa-chini-ya-masharti-makali/
No comments:
Post a Comment