Habari ya asubuhi mdau wa Opera News ni siku nyingine ya Jumamosi Agosti 01, 2020, matumaini yetu upo salama na karibu katika ujenzi wa taifa.
Tunakukaribusha katika dawati letu la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazopamba asubuhi ya leo.
Habari hizo ni Tanzania yaifungia Kenya kuleta ndege zake nchini kulikoni? Waziri ampa kibano Mkurugenzi malipo ya korosho na Makonda kukabidhi ofisi leo.
Karibu msomaji wetu;
TANZANIA YAIFUNGIA KENYA KULETA NDEGE ZAKE NCHINI
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imefuta kibai kilichokuwa kinarusha ndege za Shirika la Ndege la Kenya (KQ) kutua Tanzania.
Uamuzi huo umekuja baada ya Kenya kutoiweka Tanzania katika orodha ya nchi ambazo raia wake wataruhusiwa kuingia Kenya kuanzia Agosti 01, 2020.
Kwa mujibu wa taarifa iiyotowa jana kwa vyombo vya habari na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari, ameeeza Kenya wametangaza kuwa Agosti 01, 2020 kufungua anga lake kwa usafiri wa ndege za kimataifa kuanza kuingia nchini Kenya tangu walivyozuia Marchi 25, 2020.
WAZIRI AMPA KIBANO MKURUGENZI MALIPO YA KOROSHO
WAZIRI wa Kilimo, Japhet Hasunga, ametoa siku 14 kwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CBP), Dk. Anslem Moshi, kukamilisha malipo ya wakulima wote waliouza korosho msimu wa mwaka 2018/19.
Hasunga alitoa agizo hilo jana alipotembelea na kukagua shughuli za utendaji kazi zinazofanywa na bodi hiyo jijini hapa.
Alisema bodi hiyo ilipewa dhamana ya kununua korosho mwaka 2018 kwa niaba ya serikali na tayari serikali imeshatoa fedha zote kwa ajili ya wakulima lakini haijakamilisha malipo, hivyo ni lazima itekeleze agizo hilo ndani ya siku hizo.
“Ndani ya siku 14 sitaki kusikiliza malalamiko ya wakulima. Lazima wakulima wote wawe wamelipwa fedha zao haraka iwezekanavyo,” alisisitiza.
MAKONDA KUKABIDHI OFISI LEO
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, leo anatarajia kukabidhi ofisi kwa Mkuu wa mkoa huo Aboubakar Kunenge.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa imeeleza kuwa Makonda atafanya makabidhiano hayo ya ofisi majira ya saa 7 mchana jijini Dar es Salaam.
source http://www.bongoleo.com/2020/08/01/dondoo-za-leo-tanzania-yaifungia-kenya-kuleta-ndege-zake-nchini-waziri-ampa-kibano-mkurugenzi-malipo-ya-korosho-na-makonda-kukabidhi-ofisi-leo/
No comments:
Post a Comment