Polisi wameanzisha uchunguzi katika kisa hicho kubaini chanzo. Picha: Hisani
Vijana hao walijihami kwa silaha, panga na rungu
Waliwavamia wafanyikazi katika afisi za kaunti ya Kisumu na kuharibu vifaa vingi
Walilalamikia ubaguzi katika nafasi za ajira
Kulizuka sokomoko katika mkutano wa bodi ya umma mjini Kisumu huku vijana wenye mori waliojihami kwa silaha wakiuvuruga mkutano huo wakitaka nafasi za ajira.
Vijana hao wenye mori wakiongozwa na naibu mwenyekiti wa chama cha ODM katika eneo hilo Kennedy Ajwang walivamia afisi hizo mwendo wa 10am Jumatatu, Agosti 3 na kuwajeruhi wafanyikazi.
Kulingana na jarida la Daily Nation, vijana hao walilalamikia kile walichokitaja kama ubaguzi katika kuajiri wakusanyaji ushuru.
Vijana hao walivunjilia mlango ya afisi moja na kuanza kukata kata mafaili kwa panga zao kwa hasira.
Vijana hao walitaka kupewa barua za kuandikwa kazi hapo hapo wakisema kuwa baadhi ya maafisa katika kaunti hiyo walikuwa wakiwanyima nafasi za ajira na kuwapa jamaa zao.
Inadaiwa kuwa jamaa aliyeongoza uvamizi huo alikuwa mmoja wa wafanyikazi wa kaunti na aliamua kuupanga uvamizi huo kuwashinikiza maafisa hao kumwandika kazi mkewe.
zaidi ya wafanyikazi watano wa kaunti walijeruhiwa katika vurugu hizo na kukimbizwa hospitalini kupata matibabu.
Polisi sasa wameanzisha uchunguzi katika kisa hicho kubaini chanzo huku waliohusika wakisakwa.
source http://www.bongoleo.com/2020/08/04/vijana-wenye-mori-wavamia-afisi-za-serikali-waumiza-mabosi-kutaka-ajira/
No comments:
Post a Comment