Monday, August 3, 2020

Dondoo za leo; Lissu na kushinda urais, Nyalandu ampa tano, Wafukia ugomvi

Habari ya asubuhi mdau wa Opera News, tunatumai u bukheri wa afya.

Karibu katika dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari nchini asubuhi ya leo.

Zinazobamba leo ni pamoja pamoja na nguvu ya Lissu kushinda uchaguzi 2020, ataweza kweli? Nyalandu ampongeza na mwisho ni juu ya

LISSU NA NGUVU YAKE

Kamati kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kiliyapitisha majina matatu kati ya wachukua fomu takribani saba waliogombea nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho.

Kisha wajumbe wa Baraza Kuu walipigia kura majina hayo na jina la Tundu Antiphas Mughwai Lissu likaibuka na ushindi wa kishindo wa kura 405 kati ya 442.

Majina mengine mawili ni Lazaro Nyalandu aliyepata kura 36.

Mwanasiasa huyu kihistoria alikuwa Chama cha Mapinduzi (CCM), akiwa Mbunge wa Singida Kaskazini. Alihudumu katika nyadhifa hiyo kwa mihula minne mfululizo tangu mwaka 2000, hadi alipotangaza kuondoka mwaka 2017 na kuhamia Chadema.

Soma zaidi>>>

NYALANDU AMPONGEZA

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Kati , Lazaro Nyalandu, amempongeza Tundu Lissu, kwa kupata ushindi mkubwa wa kugombea urais.

Nyalandu ambaye ni miongoni kwa waliochukua fomu ya kugombea urais katika uchaguzi uliofanyika jana alipata kura 36 huku Lissu akiwa amepata kura 405.

“Pongezi sana kaka mh. Tundu Lissu kwa ushindi wa kishindo ulipupata baraza kuu Chadematz kuwa mgombea urais kupitia chama chetu,” aliandika Nyalandu katika ukurasa wake wa Twitter.

Soma zaidi>>>

LADY JAYDEE , CLOUDS WAFUKIA UGOMVI

Wakuu kama kichwa kinavyooleza hapo ugomvi wa Komando huyu wa kike kwenye tasnia ya burudani ya Muziki wa Bongo Fleva umezikwa, leo tangu asubuhi bandika bandua ni ngoma tu za Lady Jay Dee zinapigwa kumpa promo kwenye tamasha lake la miaka 20 yake kwenye tasnia.

Hivi ndivyo inavyotakiwa Clouds iwape uwanja sawa wasanii wote bila kubagua tutafika mbali, sifahamu kama amelipia au bure lakini cha msingi promo kama hii ifanyike kwa wasanii wote na kwa vituo vyote itasaidia kukuza mziki.

Soma zaidi>>>



source http://www.bongoleo.com/2020/08/04/dondoo-za-leo-lissu-na-kushinda-urais-nyalandu-ampa-tano-wafukia-ugomvi/

No comments:

Post a Comment