Msanii wa muziki wa bongo fleva, Judith Wambura maarufu kwa jina la Lady JayDee amesema aliyemuimba katika wimbo wa Yahaya ni rafiki yake na baada ya ngoma hiyo kuiachia amenuna hadi sasa.
Jaydee ameyasema hayo wakati akihojiwa jana jioni na CloudsFM kipindi cha Amplified amesema story ya Yahaya ni ya kweli ilimuhusu rafiki yao.
“Story ya Yahaya niya kweli na ilikuwa inamuhusu rafiki yetu, tulitoka naye sana kwenye bata alikuwa anajua tunaishi wapi ila sisi tulikuwa hatujui anakaa wapi Yahaya ni jina lake,” alisema Jaydee
Msanii huyo alisema baada ya kuachia ngoma hiyo alinuna mpaka leo na kwamba alikuwa anafikisha ujumbe.
source http://www.bongoleo.com/2020/08/04/jaydee-amtaja-aliyemuimba-yahaya-adai-amemchunia-baada-ya-kuachia-ngoma-hiyo/
No comments:
Post a Comment