Aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema asilimia 70 ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam ni wambeya.
Makonda aliyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akikabidhi ofisi kwa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakar Kunenge.
“Ninamshukuru sana make wangu na kipenzi changu Keagan kwa kuendelea kuwa wavumilivu na kuvumilia masimango na mamneno ya hovyo na machafu yaliyotamkwa juu yao na familia yangu katika kupindi chote cha utumishi na yatakayoendelea,” amesema Makonda
Makonda aliongezea kuwa “Mimi nikamuambia maneno ndiyo mtaji wangu , kusemwa ndiyo furaha yangu, nisiposemwa mpaka najiuliza leo kuna nini mitandao imekaa kimya, hawawezi kukusema kama hauna jambo la maana na kazi yako kubwa ni kumtanguliza Mungu,” alisema Makonda.
Aidha, Makonda amesema maamuzi alilokuwa anayafanya alikuwa anashirikiana na ofisi ya wasaidizi na sio alikuwa akijifanyia mwenyewe.
Alipohojiwa na kitu gani ambacho hajakitekeleza katika utendaji wake wa kazi amesema upimaji wa tenzi dume kaya kwa kaya ili kuwafuata wananchi .
Amesema ameondoka bila kulitekeleza na kwamba ugonjwa huo sio wa aibu licha ya watu kuogopa kujitokeza katika kupima tenzi dume.
Aidha, amesema atatembea mtaa kwa mtaa kumpiga debe na kuhakikisha Rais Magufuli, wabunge na madiwani wa CCM wanashinda.
source http://www.bongoleo.com/2020/08/03/makonda-asilimia-70-ya-wakazi-wa-dar-es-salaam-ni-wambeya/
No comments:
Post a Comment