Thursday, August 6, 2020

Rais Magufuli: Tanzania hatuna Corona ndio maana tunabanana hata vitandani muendelee kubanana

Rais John Magufuli amesema watafanya kampeni kwa kumtanguliza Mungu ana amini atawalinda kama alivyowalinda kwenye ugonjwa wa Corona.

Rais Magufuli ameyasma hayo leo jijini Dodoma wakati alipochukua fomu ya kugombea urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambapo Uchaguzi unatarajia kufanyika Oktoba 28, 2020.

‘Leo Tanzania hatuna Corona ndio maana tunabanana tu hapa na hata vitandani muendelee kubanana tu… nasema mbanane kwa sababu aliyenitangulia amesema tutafanya kampeni kitanda kwa kitanda,” alisema Magufuli

Rais Magufuli amewaomba wanachama wa Chama cha Mapinduzi kujitokeza kupiga kura na kwamba ameomba nafasi ya kugombea urais kwa ajili ya kuwatumikia wanyonge.

“Wanachama wa CCM msitembee tu mkisema Magufuli ameshinda au Chama kimeshinda naomba mjitokeze kupiga kura napenda kuwathibitishia nimeomba hii nafasi sio kwa kulazimishwa ila nataka kuwatumikia wanyongea,” amesema Magufuli.



source http://www.bongoleo.com/2020/08/06/rais-magufuli-tanzania-hatuna-corona-ndio-maana-tunabanana-hata-vitandani-muendelee-kubanana/

No comments:

Post a Comment