Thursday, August 6, 2020

Mwanamke Awalipa Majambazi Kumuua Shemeji, Dili Yatibuka

What Makes A Gun Sale Private? | Guns & America

Maureen Chebet aliponea baada ya kupata sauti iliyorekodiwa kuhusu njama ya kumuua. Picha: Hisani.

Mwanamke huyo alipanga kumuua shemeji yake kufuatia mzozo wa ardhi

Mwanadada huyo alipata habari na kuwapasha polisi kabla kupatwa na majambazi hao

Polisi wamewakamata washukiwa wawili waliolipwa kutekeleza mauaji hayo

Mwanadada mmoja ameponea kifo baada ya njama iliyoundwa na mke wa nduguye kumuua kutibuka.

Kulingana na kisa hicho kilichochapishwa katika jarida la Citizen, Maureen Chebet aliponea baada ya kupata sauti iliyorekodiwa kuhusu njama ya kumuua.

Akisimulia kisa hicho, Maureen alieleza kuwa mke wa nduguye aliwalipa majambazi hao wawili TSh 60,000 kumuua na kisha kuwaahidi kuchukua baki ya TSh 40,000 baada ya kuthibitisha kuwa wametekeleza mauaji hayo.

Chebet aliponea baada ya kupata rekodi ya sauti zao walipokuwa wakipanga njama hiyo na moja kwa moja akawapasha polisi kuhusu njama hiyo.

Kenya Police officers pictured outside a police station. A naked man stormed the Embakasi Police Station on Saturday night, June 13, 2020.

Tayari majambazi hao walikuwa wamekodi gari na kulitia mafuta tayari kwa kazi hiyo. Walitaka kunikata na kunitupa msituni,’’ Chebet aliliambia Citizen.

Wawili hao walifikishwa kortini na kuachiliwa kwa dhamana ya TSh200,000 Chebet sasa akihofia maisha yake baada ya wawili hao kuachwa huru akidai kuwa anazididi kupata jumbe za tishio.

‘’ Naomba kupewa ulinzi wa polisi maana maisha yangu yamo hatarini,’’ alisema.

Akizungumza kuhusu kisa hicho, kamanda wa polisi katika kaunti ya Kisii Jebel Munene alieleza kuwa washukiwa hao waliachiliwa kwa dhamana kama njia kuzuia msongamano korokoroni  kuhusiana na mlipuko wa covid19.



source http://www.bongoleo.com/2020/08/06/mwanamke-awalipa-majambazi-kumuua-shemeji-dili-yatibuka/

No comments:

Post a Comment