Thursday, August 6, 2020

Rais Magufuli amfagilia Ndugai asema atashangaa bunge lijalo wasipompa uspika

 

Rais John Magufuli amemsifia Spika wa Bunge, Job Nduagi, kuwa amefanya kazi vizuri na alisimamia sheria ambazo zimesaidia kulinda rasilimali za nchi.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati akizungumza baada ya kuchukua fomu ya kugombea urais katika Uchaguzi Mkuu ambao utafanyika Oktoba 28, 2020.

Rais Magufuli amesema atashangaa kama bunge lijalo hawatampa uspika Ndugai.

“Ndugai nitashangaa sana kama bunge lijalo hawatakupa uspika tena, najua watasema nakupigia nakupigia kampeni lakini ndio ukweli unachapa kazi vizuri,” amesema Magufuli.



source http://www.bongoleo.com/2020/08/06/rais-magufuli-amfagilia-ndugai-asema-atashangaa-bunge-lijalo-wasipompa-uspika/

No comments:

Post a Comment