Thursday, August 6, 2020

Rais magufuli awapongeza upinzani kwa kuanza kumpigia kampeni

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, amewashukuru wapinzani kwa kuanza kumpigia kampeni mapema.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo jijini Dodoma alikwenda kuchukua fomu ya kugombea urais na kueleza kuwa wengi wao wameanza kumpa kauli za kwamba atapigiwa kura na vituo vya afya, kwa kuwa hao wanaovitumia ndiyo watakaompa kura.

“Mtu akisema nitapigiwa kura na vituo vya afya, najua ndio wameshaanza kunipigia kampeni wao na ninawashukuru sana wanaosema hivyo, maana vituo vya afya wametibiwa wanawake watanipigia kura, Wazee hata walevi walilala humo watanipigia na inanipa nguvu kwamba ushindi wa mwaka huu utakuwa mkubwa amesema Rais Magufuli.

Aliongezea kuwa “Mtu akisema hiyo meli itanipigia kura nitasema ndio sababu ile meli itabeba Watanzania watakaonipigia kura, ninaogopa, ninapata wasiwasi kwamba hao ukiwaachia inawezekana hizi meli zitapigwa mnada na madaraja watavunja wauze skrepa,” alisema Magufuli.



source http://www.bongoleo.com/2020/08/06/rais-magufuli-awapongeza-upinzanj-kwa-kuanza-kumpigia-kampeni/

No comments:

Post a Comment