Thursday, August 6, 2020

Meya Kimbe Amlipua Lijualikali “ukitaka dunia ikuelewe Omba Msamaha”

ALEX KIMBE AKABIDHI OFISI KISTARABU ASEMA HATAKI WANANCHI WAKOSE ...Aliyekuwa meya wa Iringa, Alex Kimbe amemtaka aliyekuwa mbunge wa jimbo la Kilombero (CHADEMA), Peter Lijualikali kuomba msamaha kwa wanchamadema na mungu wake kutokanana usaliti aliofanya kwenye chama hicho huku akimpigia kampeni Rais Magufuli.

Kimbe amesema hayo leo kupitia ujumbe wake aliotuma kwenye ukurasa wake wa Twitter kujibu jumbe wa Peter Lijualikali jana Agosti 5, 2020, na kumdadi mgombe urais wa CCM, John Magufuli.

“Unajipendekeza ili upewe uteuzi, ujanja ni kukaa kimya tu huwezi kusema jambo lolote kwa sasa na dunia ikakuelewa, ukitaka dunia ikuelewe ni kupiga magoti na kuomba msamaha kwa usaliti ulifanya, kwa hapo unaweza kueleweka” amendika Kimbe.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/08/06/meya-kimbe-amlipua-lijualikali-ukitaka-dunia-ikuelewe-omba-msamaha/

No comments:

Post a Comment