Wednesday, August 5, 2020

Polepole Aipasua CHADEMA Kubadilisha wimbo wa taifa

LIVE: KATIBU MWENEZI POLEPOLE ANAZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI ...Katibu wa uenezi wa chama cha mapinduzi (CCM) Humprey Polepole ameshangazwa na kitendo cha chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kubadilisha beti kwenye wimbo wa taifa wakati wa mkutano mkuu wa chama  hicho ulimalizika hivi karibani.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam leo Agosti 5, 2020 kwenye ofisi ya chama hicho ofisi ndogo za chama hicho Lumumba amesema kitendo cha chama hicho kubadilisha nyimbo hiyo ni kuvunja sheria licha ya kutokauwa na sheria rasmi inayoonyesha ouvu huo.

“Hiki nichama ambacho kabla hakijapata dola kinaanza kubadilisha wimbo wa watanzania kuwa wimbo wa chama chao, tena kwa kujimwambafai kuwa wako sahihi, huu ni wimbo unowatambulisha watanzania sio wimbo unaotambulisha chama cha mtu fulani, kwai hapa nchini kuna sheria inayosema usichukue mke wa kaka yako sasa kwa nini wao wanajiona wako sahihi” amesema Polepole.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/08/05/polepole-aipasua-chadema-kubadilisha-wimbo-wa-taifa/

No comments:

Post a Comment