Wednesday, August 5, 2020

Chanzo Cha Mlipuko wa Beirut Lebanon Chabainika, Habari Kamili

Beirut blast: Trump says explosion "a bomb of some kind" - AS.com

Kulingana na wenyeji, mlipuko wa aina hiyo ni wa kwanza katika hisotoria ya nchi ya Lebanon. Picha:Hisani

Mlipuko huo uliofanyika ghafla Beirut ilisababisha vifo vya wengi  na kuwaacha wengine kwa majeraha mabaya

Mlipuko huo uliofanyika mara mbili uliangusha majumba, kuharibu madaraja na kuangusha magari

Inadaiwa kuwa kilichosababaisha mlipuko huo ni mzigo wa ‘ammoniam nitrate, bidhaa inayotumika kuunda mbolea na mabomu

Dunia inaendelea kuomboleza vifo vya wanachi wa Lebanon waliopoteza maisha kufuatia milipuko ya ajabu iliyosababisha vifo na uharibu makubwa usiku Jumanne, Agosti 4 katika mji wa Beirut.

Mlipuko huo ambao ulifanyika ghafla uliwaua makumi ya watu, wengi kujeruhiwa vibaya na mali ya thamani kubwa kuharibiwa.

Kulingana na wenyeji, mlipuko wa aina hiyo ni wa kwanza katika hisotoria ya nchi ya Lebanon.

Kwa mujibu wa jarida la New York Times, mlipuko huo ulitokana na vilipuzi ambavyo mamlaka maalum ilikuwa imekamata miaka michache iliyopita na kuweka katika eneo hilo kama njia kuhifadhi.

Beirut blast: Tracing the explosives that tore the capital apart ...

Mlipuko huo ulifanyika mara mbili, wa pili ukiwa mkubwa zaidi. Picha: Hisani

Inadaiwa kuwa shehena hiyo ilkuwa na ‘Amonium Nitrate’ ambayo huwa kiungo kikuu katika kuunda mbolea na mabomu.

Kiongozi mmoja wa hadhi ya juu jeshini Lebanon ameitaka mamlaka ya nchi hiyo kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua za kisheria wahusika. Hii ni baada ya kubainika kuwa shehena hiyo ya ammonium Nitrate ya tani 2,750 iliyosababisha ajali hiyo ilikuwa imehifadhiwa katika jumba hilo kwa zaidi ya miaka sita.

Akizungumza awali kuhusiana na kisa hicho, waziri mkuu wa Lebanon Bw. Diab alisema kuwa mzigo huo ulikuwa katika jumba hilo tangu 2014 na akataka wahusika kuchukuliwa hatua za kisheria.

Kulingana na jarida la Ney York Times, zaidi ya watu 70 wameripotiwa kufariki kufuatia mkasa huo huku maelfu wakijeruhiwa.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/08/05/chanzo-cha-mlipuko-wa-beirut-lebanon-chabainika-habari-kamili/

No comments:

Post a Comment