Thursday, August 6, 2020

“Hatujashinda Tusitembee Kifua Mbele” Magufuli

Mgombea wa urasi kwa tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM), Dkt John Magufuli amewataka wanachama wa chama hicho kujitokeza kwa wingi kupiga kura ili kuhakikisha anashinnda kwa kishindo kwenye uchaguzi mkuu ujao mapema mwezi Oktoba.

Akizungumza na wanaCCM baada ya kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo kwenye ofisi za tume ya uchaguzi jijini Dodoma leo Agosti 6, 2020 amesema wanaCCM hawatakiwi kutembea kifua mbele kujiamini kuwa wameshinda bila kujitokeza kupiga kura.

  “Tusitembee kifua mbele kusema tumeshinda bila kupiga kura tutapunguza hizo kura nawaomba mjitokeze kwa wingi sana siku ya kupiga kura ili tushinde kwa kishindo maana bila kupiga kura haruwezi kusinda” amesema.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/08/06/hatujashinda-tusitembee-kifua-mbele-magufuli/

No comments:

Post a Comment