Thursday, August 6, 2020

Dozen Afunguka Kuondoka Clouds Kama Ruge Angekuwa Hai

B Dozen "Niseme tu Ukweli Aslay ni Msumbufu Sana Fiesta Ana ...Mtangazaji maarufu nchini, Hamis Mandi  (B Dozen) ameweka wazi kuwa kama aliyekuwa mkurugenzi wa vipindi wa kituo cha habari cha Clouds Fm, Ruge Mutahaba angekuwa hai asingeondoka kwenye kituo hicho.

Akizungumza kwenye kipindi cha Gerezani kinachorushwa na kituo cha televisheni cha ETV na kudai kuwa mapenzi yake kwenye tasnia ya burudani ndio yamefanya ahame kutoka clouds Fm na kujiunga na Efm.

“Nafikiri kama angekuwepo nisingeondoka Clouds, lakini mimi ni mtu ninayependa zaidi burudani kuliko kutangaza kwa hiyo Majizzo alivyonipa mipango yake nikaona huku ndiko kuna   Future” amesema Hamis.

Dozen alitambulishwa rasmi kwenye kituo cha E fm mapema Mwezi wa Juni baada ya kudumu clouds Fm kwa takribani miaka 9.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/08/06/dozen-afunguka-kuondoka-clouds-kama-ruge-angekuwa-hai/

No comments:

Post a Comment