Thursday, August 6, 2020

Manchester City Yamsaini Nyota wa Bournemuth kwa TSh 112 Milioni

Official: Manchester City sign Nathan Ake for KSh 5.6 billion from Bournemouth

Guardiola amsaini Nathan Ake. Picha:Hisani

Nathan Ake alitia saini dili ya miaka mitano na Man City

Nyota huyo anatarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa kiafya Alhamisi , Agosti 6

Ake amekuwa mchezaji wa pili kusainiwa na klabu hiyo baada ya Ferran Tores

Ni rasmi kuwa mchezaji sugu wa kiungo cha ulinzi katika klabu ya Bournemouth sasa amehamia Man City siku chache tu baada msimu kumilika.

Nyota huyo ambaye amesaini dili ya miaka mitano anadaiwa kununuliwa kwa TSh 112 Milioni (£40million).

Ake ambaye alichezea klabu yake mara 29 sasa atakuwa mwana klabu ya Man City baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kiafya Alhamisi, Agosti 6.

Mchezaji huyo atakuwa wa pili kutiwa saini na Manchester City chini ya saa 24 baada ya kumsaini Ferran Tores wa Valencia.

Ake alionyesha furaha kubwa kujiunga na klabu hiyo akiwa na matumaini makubwa.

‘’City imekuwa klabu bora England katika mwongo mzima. Kuwa hapa ilikuwa ndoto kwangu.  Hii ni klabu ya hadhi ya juu na yenye wachezaji wa ajabu. Kila unapogeuka katika timu hii, ni majina makubwa,’’ alisema.

Ake alijiunga na Bournemouth alipotoka Chelsea 2017. Katika Man City, mchezaji huyo atakuwa wa manufaa makubwa haswa na kutokana na udhaufu ambao umeikumba kiungo cha ulinzi wa klabu hiyo.



source http://www.bongoleo.com/2020/08/06/manchester-city-yamsaini-nyota-wa-bournemuth-kwa-tsh-112-milioni/

No comments:

Post a Comment