Thursday, August 6, 2020

Je unajua madhara utakayoyapata endapo mpenzi wako hatakufikisha kileleni

 

Habari ya muda huu msomaji wangu karibu katika ukurasa wetu wa mahusiano.

Mada yetu ya leo ningependa tueleweshana mambo machache na pia uelewe umuhimu wa kufika kileleni unapokuwa kwenye ule mchezo wa kitandani.

Kuna mambo mbalimbali ambayo yanachangia mwanamke kushindwa kufika kileleni na sababu kubwa husababishwa na maandalizi hafifu.

Kunapokosekana maandalizi ya kutosha husababisha mwanamke kushindwa kufika kileleni.

Tunaposema mwanamke au mwanaume amefika kileleni katika penzi ni pale amefika kiwango cha juu cha msisimko na raha wakati wanafanya mapenzi.

Mwanaume huanza kusisimka katika sehemu ya mbele yaani kwenye uume wake na mwanamke huwa na sehemu maalumu.

Msisimko hubebwa na mishipa ya fahamu ya kiuno, uti wa mgongo hadi katika ubongo ambapo kiwango cha juu hufikiwa na mwanaume hutoa manii na mwanamke hutoa majimaji sehemu ya siri.

Chanzo kikuu kinachoweza kumsababishia mwanamke asifike kileleni au achelewe kufika hapo ni sababu za kimazingira na kisaikolojia.

Zipo sababu nyingine za magonjwa au mifumo ya mwili mfano, mfumo wa fahamu na homoni.

Kiasi kikubwa cha tatizo hili hutokana na matatizo yanayomzunguka mwanamke kama vile, maandalizi duni ya tendo la ndoa kwa kutozingatia kanuni na mwanamke kuingiliwa kabla ya kuwa tayari na hii inaweza kuwa ni kila mara.

Kutokuamsha viungo vyake vya uzazi kwa ajili ya tendo (Insufficient foreplay) tatizo jingine ni wote wawili mume na mke kutojua mapenzi na kazi ya viungo vyao vya uzazi.

Eneo hilo ni muhimu ukatenga muda kwa ajili ya kuandaana hata nusu saa ndipo muanze kufanya mapenzi na sio kumkurupusha mwenzako vua nguo na kuanza kuingiza uume wako.

Mapenzi hayapo hivyo lazimu muanze kutomasana yale maeneo ambayo yanasisimua na kuanza kupata nyege ili muelekeo upepo mwingine wa kuanza kupeperusha safari ya mahaba.

ATHARI ZA TATIZO

Mwanamke ambaye hafiki kileleni wakati akiwa anafanya mapenzi anaweza kupoteza hamu ya kufanya mapenzi kutokana hapati huo msisimuko ambao wengine wanaupata.

Ni muhimu kuelewa kuwa mwanamke ambaye hafiki kileleni hupata hamu kama kawaida pale tatizo linapoanza , pia hupata msisimko ambao haufiki mshindo kutokana na kukatizwa na mumewe endapo mumewe anawahi kumaliza tendo.

Ukiendelea na hali hiyo mara kwa mara mwanamke huyo hupoteza kabisa uwezo wa kumaliza tendo kwa mshindo au kufikia kileleni.

Tatizo linapoendelea husababisha mwanamke awe anapata maumivu wakati wa tendo la ndoa.

Maumivu haya hutokana na woga au wasiwasi hivyo kusababisha uke uwe mkavu na misuli yake hubana hivyo hata uume unashindwa kupenya.

MATIBABU

Daktari atakuelekeza njia mbalimbali za mguso wa kuamsha hisia na msisimko ili kukuwezesha kufikia kileleni na kurudisha furaha yako na kama hujawahi kuipata basi utaipata.

Njia nyingine ni kupata elimu na upeo kuhusu mapenzi, tiba nyingine ni za kisaikolojia kutambua na jinsi ya kuepuka migongano katika mahusiano ya kimapenzi.



source http://www.bongoleo.com/2020/08/06/je-unajua-madhara-utakayoyapata-endapo-mpenzi-wako-hatakufikisha-kileleni/

No comments:

Post a Comment