Thursday, August 6, 2020

Vilabu EPL Vyapinga Mabadiliko Wachezaji Watano


Vilabu vinavyoshiriki ligi kuu nchii Uingereza zimepiga kura ya kukataa kufanyika kwa mabadiliko ya wachezaji 5 kwenye msimu mpya 2020/21 wa ligi bara unaotarajia kuanza mapema mwenzi September.

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa na SkySport vilabu hivyo vimedai kuwa mabadiliko ya wachezaji watano zitavipa nguvu kubwa zaidi vilabu vikubwa na kuvione vilabu vyenye vikosi dhaifu.

Sheria ya Mabadiliko ya watu watano kwenye mechi moja ilianzishwa mapema mwezi Juni baada ya kurejea kwa ligi nchini Uingereza baada ya kusimama kwa muda kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Corona.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/08/06/vilabu-epl-vyapinga-mabadiliko-wachezaji-watano/

No comments:

Post a Comment