Monday, August 3, 2020

Chifu, Wenyeji Waichoma Nyumba ya Jamaa kwa kumuoa Mke Aliyemshida Umri

 

25 Year Old Man Throws Mother Into Burning House And Locks Doors ...

Inadaiwa kuwa wenyeji hao waliiteketeza nyumba ya Okinyi baada ya kuagizwa na chifu. Picha: Hisani

Joash Okinyi amedai kuwa chifu wa eneo hilo ndiye aliyewaelekeza vijana kuiteketeza nyumba yake

Kulingana na Okinyi, alitofautiana na ndugu zake waliotaka amtoroshe mkewe kwa kwa kumzidi umri

Rudi Okinyi amemzidi mumewe kwa miaka saba

Joash Okinyi, mkazi wa Birongo, eneo bunge la Nyaribari, kaunti ya Kisii ameitaka serikali kumpa haki baada ya wenyeji kuichoma nyumba yake.

Katika kisa hicho kilichofanyika Ijumaa, Julai 31, inadaiwa kuwa wenyeji hao waliiteketeza nyumba ya Okinyi baada ya kuagizwa na chifu.

Okinyi ameeleza kuwa alitofautiana  na jamaa wake waliotaka ampe talaka  mkewe kwa kuwa na umri mkubwa kumshinda hata baada ya kujaliwa watoto watano.

Katika mahojiano na jarida la Star, Okinyi alieleza kuwa amekuwa akishinikizwa kila mara kumtaliki mkewe ambaye amemzidi kwa miaka saba suala ambalo amalikitaa kabisa.

Kulingana naye, siku ya kisa, Zachary Nyariku ambaye ndiye Chifu wa eneo hilo aliandaa mkutano na wenyeji na kuwaagiza kuichoma nyumba yake pamoja na mali yake yote.

Dormitory at Elsa Academy, Kisii razed in night fire » Capital News

Wawili hao walikuwa wamejaliwa watano. Picha: Hisani

‘’Nimekuwa na mvutano na ndugu zangu na majirani waliodai kuwa nahitaji kumuoa mke mwengine mdogo. Kukataa kwangu kumenisababishia hasara hii. Sijawahi kuwa na shida naye,’’ Okinyi alisema.

Mkewe, Rudi Okinyi alisisitiza kauli hiyo akieleza kuwa wameishi kwa miaka 15 na Okinyi bila mzozo wowote.

‘’ Nimeishi naye kwa miaka 15 na kutkuwa tukiwalea wana wetu watano bila tashwishi,’’ Mkewe alisisitiza.

Okinyi ameitaka serikali kuingilia kati kuona kuwa anafidiwa kufuatia hasara hiyo na kuwezeshwa kuishi na mkewe bla kushurutishwa.



source http://www.bongoleo.com/2020/08/03/chifu-wenyeji-waichoma-nyumba-ya-jamaa-kwa-kumuoa-mke-aliyemshida-umri/

No comments:

Post a Comment