Wednesday, August 5, 2020

Lissu: Rais Magufuli amekiuka taratibu za uchaguzi

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu amesema ukionekana unatoa fedha wakati ni mgombea wa urais hiyo ni rushwa.

“Ukishatoa milioni 5 wakati umeshapitishea kuwa mgombea wa urais ni rushwa na hata ukitoa pesa ya kununua madawati kwa taratibu za uchaguzi inahesabika kuwa ni rushwa,”

Lissu amesema kwenye fomu ya mapingamizi kwenye sababu 16 la 16 Rais Magufuli amekiuka mambo yaliyokatazwa.

“Moja wapi ni rushwa maana ukishaingia kwenye uchaguzi huruhusiwi kutoa rushwa, Magufuli akiwa anataka kumzika Mkapa Lupaso, alifanya nini Kibiti?,”

“Nani aliyesema kwamba CCM hawawezi kuwekewa mapingamizi? Nano aliyesema mgombea urais wa CCM Magufuli hawezi kuwekewa mapingamizi,” alihoji Lissu



source http://www.bongoleo.com/2020/08/05/lissu-rais-magufuli-amekiuka-taratibu-za-uchaguzi/

No comments:

Post a Comment