Wednesday, August 5, 2020

Bibi wa Miaka 62 Kutumikia Kifungo cha Miaka 35 kwa Wizi wa Mabavu

62-year-old grandmother sentenced to 35 years in jail for robbery of vehicles

Joyce alifuatwa na kukamatwa baada ya wengi kupiga ripoti kuhusu alivyoanyanganya magari. Picha: Hisani.

Joyce Wairimu Kariuki alikuwa ameiba magari kadhaa kati ya 2018-2019

Alikamatwa Aprili 23, 2019 baada ya kuiba gari aina ya Prado

Si mara ya kwanza Joyce anatumikia kifungo kwa wizi wa mabavu

Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 62 atalazimika kutumikia kifungo cha miaka 35 baada ya kupatikana na hatia ya wizi wa magari.

Joyce Wairimu Kariuki ambaye pia alikuwa mfungwa katika gereza la Shimo la Tewa alikamatwa Aprili 23, 2019 na kufikishwa mbele ya mahakama Loitoktok alikopatikana na hatia ya wizi wa mabavu.

Kulingana na mkurugenzi wa upelelezi, Joyce alifuatwa na kukamatwa baada ya wengi kupiga ripoti kuhusu alivyoanyanganya magari.

‘’ Kufuaia ripoti kadhaa kuhusu wizi wa magari haswa malori  katika eneo la Nakuru, Nairobi na Mombasa kati ya 2018 na 2019,  DCI Kenya ilimtafuta na kumkamata mshukiwa huyo licha ya kumaliza kifungo cha miaka 15,’’ alisema DCI.

62-year-old grandmother sentenced to 35 years in jail for robbery of vehicles

Joyce alikuwa mwizi wa malori. Picha: Hisani

Baadhi walishangaa na kumuonea huruma bibi huyo ambaye sasa atakumikia jumla ya kifungo cha miaka 60 gerezani wengi wakimshambulia na kutaka apewa adhabu zaidi.

Visa vya wizi wa magari vimepanda vimezidi  kupanda, DCI akichukua nafasi ya kuonya wanaohusika kuhusu adhabu kali inayowasubiri.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/08/05/bibi-wa-miaka-62-kutumikia-kifungo-cha-miaka-35-kwa-wizi-wa-mabavu/

No comments:

Post a Comment