Thursday, August 6, 2020

KENYA: Zaidi ya Watu 20 wa Familia Moja Waambukizwa COVID19, Mmoja Afariki Ghafla

48 members of Migori family test positive for COVID-19, one dies

Kila mmoja katika familia hiyo ametiwa karantini baada ya kupatikana na virusi. Picha: Hisani

Mmoja katika familia hiyo alifariki kutokana na covid19 muda mfupi baada ya kulazwa hospitalini

Kulingana na Gordon Ogolla aliyetoa habari hizo, mamake mwenye umri wa miaka 80 yuko kwenye ICU

Kila mmoja katika familia hiyo ametiwa karantini baada ya kupatikana na virusi

Good afternoon great friends. I want to plead with all of us to spread the gospel of the reality of this…

Posted by Wachite Morgan on Tuesday, 4 August 2020

Zaidi ya watu 20 wa familia moja wameambukizwa virusi hatari vya corona katika kaunti ya Migori.

Kulingana na Gordon Ogola ambaye ni wakili mjini Nakuru, kijiji kizima cha Godngoche kiliambukizwa virusi hivyo hatari baada ya mmoja wao kusafiri kutoka Nairobi.

Wakili huyo alifunguka kuhusu kisa hicho alipobainisha kuwa nduguye mwenye umri wa miaka 61 alifariki saa chache baada ya kulazwa hospitalini alipopatikana na virusi hivyo.

Kenya bans public events after first case of coronavirus | Kenya ...

‘’ Wiki moja iliyopita imekuwa ya machungu na majonzi kwa familia ya zima ya Ogolla. Chini ya siku saba, tuna zaidi ya maambukizi 48 akiwemo mamangu mwenye umri wa miaka 80.’’ Alisema.

Ogolla alieleza kuwa mamake amekuwa katika ICU kwa siku tano baada ya kupatikana na virusi hivyo, hali yake ikizidi kuzorota.

Aidha, alieleza kuwa kila mmoja aliyetangamana na mamake huyo sasa ameambukizwa covid19 akiwemo mama wa kambo, wapwa pamoja na wafanyikazi.

Akizungumza na jarida la People Daily, Ogola alisema kuwa mamake ndiye aliyekuwa wa kwanza kuambukizwa virusi hivyo kabla kusambaa kwa familia na kijiji kizima.

‘’Nataka dunia nzima ijue ukweli; janga hili lipo nasi na ni hatari,’’ Ogola alisema.

Licha ya Kenya kuvamiwa pakubwa na virusi hivyo, Tanzania nzima imesalia tisti Rais Magufuli akieleza kuwa virusi hivyo havipo. Kulingana naye, Mungu ameikinga na kuwaponya Watanzania walioambukizwa.



source http://www.bongoleo.com/2020/08/06/kenya-zaidi-ya-watu-20-wa-familia-moja-waambukizwa-covid19-mmoja-afariki-ghafla/

No comments:

Post a Comment