Wednesday, August 5, 2020

Dondoo za leo: Panga kali watoa rushwa ubunge CCM, Rais Magufuli kuchukua fomu leo ya kugombea urais na mwanafunzi abuni gari shamba la bei nafuu

Habari ya asubuhi mdau wa Opera News, tunatumai u bukheri wa afya.

Karibu katika dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari asubuhi ya leo.

Habari hizo ni panga kali kutembezwa kwa waliotoa rushwa ubunge CCM, Rais John Magufuli kuchukua fomu ya kugombea urais leo na Mwanafunzi abuni gari shamba la bei nafuu.

Karibu msomaji wetu;

PANGA KALI WATOA RUSHWA UBUNGE CCM

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema wanachama wake wote waliojihusisha na rushwa wakati wa mchakato wa kuwania kuteuliwa ubunge na udiwani, watakatwa wakati wa kuteua watakaogombea nafasi hizo.

Vikao vya CCM vinatarajiwa kufanyika wakati wowote kuanzia sasa kuteua wanachama watakaopeperusha bendera ya chama hicho kwenye nafasi za ubunge, uwakilishi kwa upande wa Zanzibar na udiwani katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 28, mwaka huu.

Katika kura za maoni zilizofanyika hivi karibuni katika maeneo mbalimbali nchini, kuliibuka madai ya baadhi ya wanachama kujihusisha na vitendo vya rushwa. Kutokana na hali hiyo, CCM imesema walioingia katika mkumbo huo watachukuliwa hatua ikiwamo kutopewa nafasi ya kugombea.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Itikadi na Uenezi ya CCM, Humphrey Polepole, alisema jana kuwa wanazo taarifa za watu wanachama waliotumia rushwa katika mchakato huo na kwamba watawaadabisha na kuwashangaza.

Soma zaidi

RAIS MAGUFULI KUCHUKUA FOMU LEO YA KUGOMBEA URAIS

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Dkt. Magufuli,  leo 06 Agosti, 2020 atachukua fomu ya Kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM katika Ofisi za Makao Makuu ya Tume ya Taifa ya UchaguziTanzania (NEC) Njedengwa Jijini Dodoma.

Rais Magufuli atachukua fomu majira ya Saa tatu asubuhi na atasindikizwa na watu wachache wakiwemo viongozi wakuu wa Chama, ikiwa ni kutekeleza matakwa na maelekezo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Rais Magufuli anachukua fomu hiyo ili kugombea Urais kwa kipindi cha Pili katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 28 Oktoba, 2020.

Soma zaidi

MWANAFUNZI ABUNI GARI SHAMBA LA BEI NAFUU

MWANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Musa Doto amebuni na kutengeneza hatua ya awali ya gari shamba litakalokuwa na uwezo wa kufanya kazi nane tofauti zinazohusu kilimo kwa ajili ya matumizi ya kumpatia unafuu mkulima mdogo nchini.

Doto, ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa uhandisi, umwagiliaji na rasilimali maji wa chuo hicho amebuni gari hilo akiwalenga wakulima wadogo ambao hawana kipato kikubwa cha kununua matreta yanayouzwa kati ya Sh milioni 30 hadi 40.

Soma zaidi

 



source http://www.bongoleo.com/2020/08/06/dondoo-za-leo-panga-kali-watoa-rushwa-ubunge-ccm-rais-magufuli-kuchukua-fomu-leo-ya-kugombea-urais-na-mwanafunzi-abuni-gari-shamba-la-bei-nafuu/

No comments:

Post a Comment