Thursday, August 6, 2020

Dkt Bashiru Awarushia Vijembe Akina Membe


Katibu mkuu wa chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt Bashiru Ally amerusha kijenge kwa chama cha ACT- Wazalendo juu ya msemo wao wa kazi na bata kuelekea kwenye uchaguzi mkuu ujao mwezi Oktoba.

Akizungumza baada ya kumgombea urasi wa chama hicho Dkt John Magufuli kuchukua fomu kwenye ofisi za tume ya uchaguzi Dkt Bashiru amesema kazi ya kutafsiri msemo huo ana waachia wananchi wenyewe.

“Msimu huu tutasikia misemo mingi sana nimeshasikia msemo wa kazi na bata sasa sijui watafanya kazi wakiwa wanakula bata au watafanya kazi alafu walale na bata au sijui watafanya kazi watuachie sisi bata au watafanyakazi na bata mimi hilo sijui nawaachia nyinyi” Bashiru Ally amesema.

Zoezi ka kuchukua fomu kwa wagombea wa Urais kwenye uchaguzi mkuu ujao limefunguliwa rasmi jana Agosti 5, 2020 na vyama vyote vitakavyoshiriki uchaguzi vinayakiwa kuchukua gomi hizo kabla ya Agosti 25.



source http://www.bongoleo.com/2020/08/06/dkt-bashiru-awarushia-vijembe-akina-membe/

No comments:

Post a Comment