Tuesday, August 4, 2020

Lady Jaydee asema hawezi kurudisha penzi lake kwa Gadner

Msanii wa muziki wa bongo fleva, Judith Wambura ambaye ni maarufu kwa jina la Lady Jaydee  amesema hawezi kurudusha penzi lake kwa mtangazaji wa Clouds Gadner Habash ambaye alifunga naye ndoa.

Msanii huyo ameyasema hayo jana wakati akihojiwa na Clouds FM ambapo alieleza kuwa ameishi naye katika ndoa kwa kipindi cha miaka tisa.

Alisema kila mmoja ana mapungufu yake ila kwa ubinadamu ni mtu mwenye utu.

“Siwezi kuusemea moyo wake lakini kwa upande wangu nimeshafunga hiyo chapter ya kurudisha mapenzi ni marafiki tu  ingawa mwanzoni tulichukiana ni kawaida mkiachana,” alisema Jaydee

 



source http://www.bongoleo.com/2020/08/04/lady-jaydee-asema-hawezi-kurudisha-penzi-lake-kwa-gadner/

No comments:

Post a Comment