Thursday, August 6, 2020

Fatma Karume : Sijaelekezwa kumchagua Magufuli

Wakili wa kujitegemea, Fatma Karume, amesema yeye ni mtanzania na kwamba hajaelekezwa kumchagua Rais John Magufuli.

Fatma Karume aliandika ujumbe huo akimjibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamis Kigwangalla baada ya kuweka ujumbe huu.

“Safari inaendelea. Mungu awe nawe kwenye kampeni zinazokuja. Tunatimiza wajibu kukutaka kikatiba kugombea lakini Watanzania walishaelekezwa na Mungu kukuchagua kabla ya kuzaliwa! Natamani ningekuwepo kukusindikiza kuchukua fomu leo, lakini acha nikuombee dua tu. # hapakazitu,” aliandika Kigwangalla.

Baada ya ujumbe huo, Fatma alikuja kumjibu na kusema Mungu kamuelekeza saali, aende Mecca, asiabudu masanamu na kwenye msahafu na hadithi hajaona jina la Magufuli.

“Pia nimesoma biblia na ninakuhakikishia jina lake halimo,”aliandika Fatma.



source http://www.bongoleo.com/2020/08/06/fatma-karume-sijaelekezwa-kumchagua-magufuli/

No comments:

Post a Comment