Thursday, August 6, 2020

Jamaa Aliyetekwa Nyara Adondoka Gari Likienda Kasi, Watekaji Wamwadama na Kumuua kwa Risasi

Books to Read If You Love True Crime | Penguin Random House

Watekaji nyara walimfuata hadi nyumba alimoingia na kumfyatulia risasi kabla kuondoka upesi. Picha: Hisani

Watekaji Nyara hao walifika nyumbani kwake na kujidai kuwa maafisa wa polisi waliokuja kumkamata

Wakiwa njiani, walimueleza kuwa wangemuua kwa kukataa kumuachia nduguye kipande maalum cha ardhi

Aliruka kutoka kwa gari hilo na kuingia kwenye boma moja karibu na barabara kutafuta usaidizi

Watekaji nyara walimfuata hadi nyumba alimoingia na kumfyatulia risasi kabla kuondoka mbio

Kijiji cha Ebwaliri, Mumias, kaunti ya Kakamega kimegubika majonzi na mchanganyiko baada ya jamaa mmoja kuuliwa eneo hilo katika njia ya kutatanisha.

Kulingana na jarida la K24, Jamaa mwenye umri wa makamo aliuliwa na watekaji nyara hata baada ya kuruka kutoka kwenye gari lao kutafuta msaada.

Inadaiwa kuwa watekaji nyara hao walifika nyumbani kwa bwana huyo na kumkamata wakidai kuwa wao ni maafisa wa upelelezi.

Police suspect that a land tussle pitting the deceased against one of his brothers could have led to the fatal attack. [PHOTO | FILE]

Baada ya kumtia kwenye gari lao, waliendesha kasi bila kujua anakopelekwa. Walipokuwa njiani, aliambiwa kuwa walikuwa wanaenda kumuua kwa kukataa kuacha kuzozania kipande cha ardhi na nduguye.

Ghafla, jamaa huyu aliruka kutoka kwenye gari hilo na kutimka mbio hadi katika boma moja karibu na barabara hiyo kujiokoa.

Watekaji nyara hao watatu walisimamisha gari na kumfuata pole pole hadi boma hilo na kumuagiza atoke nje alikokuwa amejificha.

Alikatalia ndani ya nyumba moja humo huku akipiga kelele kuomba usaidizi. Majambazi hao walichukua bunduki za na kuuvunja mlango wa nyumba hiyo kabla kumfyatulia risasi na kumuua pao hapo.

Huku habari zikienea kuwa nduguye bwana huyo ndiye aliyewakodisha majambazi hao, wenyeji wenye mori waliamka Alhamisi, Agosti 6 na kuichoma boma yake kama kiasi.

Akithibitisa kisa hicho, OCPD wa Mumias David Ndirangu alieleza kuwa mwili wa marehemu ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Kakamega huku uchunguzi ukianzishwa kuwakamata waliohusika.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/08/06/jamaa-aliyetekwa-nyara-adondoka-gari-likienda-kasi-watekaji-wamwadama-na-kumuua-kwa-risasi/

No comments:

Post a Comment