Tuesday, August 4, 2020

Dondoo za Leo: Ni Lissu dhidi ya JPM urais, Chadema yaja na mfumo mpya waliokimbia kuitamani na Serikali yamwaga ajila za walimu 12,000.

Habari ya asubuhi mdau wa Opera News, tunatumai u bukheri wa afya.

Karibu katika dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari nchini asubuhi ya leo.

Zinazobamba leo ni pamoja na Ni Lissu dhidi ya JPM urais, Chadema yaja na mfumo mpya waliokimbia kuitamani na Serikali yamwaga ajila za walimu 12,000.

Ni Lissu dhidi ya JPMUchaguzi Tanzania 2020:Tundu Lissu kupeperusha bendera ya Chadema ...

Makamu mwenyekiti kitu wa chama cha Demoyns na Maendeleo  (CHADEMA) Tundu Lissu amechaguliwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa chama hicho kuwania uraisi kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Lissu ambaye amepitishwa bila kupingwa na wajumbe hai ataipeperusha ya CHADEMA kwenye uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mapema mwezi Oktoba.

Lissu amemteua aliyewahi kuwa naibu katibu mkuu wa chama hicho, Salum Mwalim kuwa mgombea mwenza kwenye nafasi hiyo ya juu zaidi kisaisa nchini, Pia chama hicho kimempitisha Said Issa Mohamed kuwa mgombea wa urais kwa upande wa Zanzibar.

SOMA ZAIDI>>>>>>>

CHADEMA Yaja  Na Mfumo MpyaImage

Mwenyekiti wa chama cha Demorasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe amezindua rasmi mfumo mpya wa kidigitali wa chama hicho utakao wawezesha wa wanachama wa chama hicho kujiunga na kupata kadi zao kwa njia ya mtandao bila kufika kwenye ofisiza za chama hicho.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mfumo huo mpya wa kidigitali Mbowe amesema mfumo huo utakuza chama chao na utapima utedaji kazi wa wanachama wake kupitia njia za kigitali.

SOMA ZAIDI>>>>>>>

Serikali Yamwaga Ajira 12,000 MpyaUhaba wa walimu unavyoua elimu

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo, alitangaza taarifa hiyo njema kwa kada hiyo alipohutubia kwenye Siku ya TAMISEMI jijini hapa na kubainisha mafanikio kwa kipindi cha miaka mitano katika sekta ya elimu.

Alisema kwa kipindi cha miaka mitano, walimu zaidi ya 18,000 wameajiriwa na kupelekwa shule za msingi na sekondari na kwamba wanaendelea na mchakato wa kutoa ajira zingine 12,000 zilizoelekezwa na Rais John Magufuli.

SOMA ZAIDI>>>>>>>

 

Kumalizia dondoo zetu, tuangazie suala la kujipima HIV mwenyewe ukiwa nyumbani

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tayari limeipitisha rasmi sheria inayompa mamlaka, mtu kujipima mwenyewe Virusi vya Ukimwi kwa kutumia sampuli zinazotoka kwenye kinywa, pamoja na sheria inayoruhusu kijana kuanzia miaka 15, kupima Ukimwi bila ridhaa ya mzazi.

Sheria hiyo imepitishwa jana Novemba 12, 2019, na kwamba sheria hiyo itasaidia watu kujitambua hali zao mapema, hususani wanaume na kundi la vijana, ambalo kwa sasa ndilo linaloongoza kuwa na waathirika wengi wa ugonjwa huo.

Wadau wamekua na maoni tofauti ambapo baadhi yao wameipongeza hatua hiyo huku wengine wakihisi ni hatarishi. Nini maoni yako mdau wetu, upo tayari kujipima mwenyewe maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi?



source http://www.bongoleo.com/2020/08/05/dondoo-za-leo-ni-lissu-dhidi-ya-jpm-urais-chadema-yaja-na-mfumo-mpya-waliokimbia-kuitamani-na-serikali-yamwaga-ajila-za-walimu-12000/

No comments:

Post a Comment