Tuesday, August 4, 2020

CHADEMA Yaja na Mfumo Mpya “Waliokimbia Watatamani Kurudi”

ImageMwenyekiti wa chama cha Demorasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe amezindua rasmi mfumo mpya wa kidigitali wa chama hicho utakao wawezesha wa wanachama wa chama hicho kujiunga na kupata kadi zao kwa njia ya mtandao bila kufika kwenye ofisiza za chama hicho.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mfumo huo mpya wa kidigitali Mbowe amesema mfumo huo utakuza chama chao na utapima utedaji kazi wa wanachama wake kupitia njia za kigitali.

“Wanaofanya kazi watapimwa kwa mfumo wa ki-digitali, Chama kikazidi kukua, wale waliokimbia Chama hiki wakatamani kurudi. Asanteni kwa  kuja kwenye Mkutano Mkuu wa Chama, nawatakia ushindi mnono katika uchaguzi” amesema Mbowe.

Chadema imezindua mfumo huo wa kidigtali kwa leong la kutizama ukuaji wa chama na utekelezani wa ilani ya chama hichi maeneo mbalimbali nchini bila kuwa na usumbufu wa kutembelea matawi.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/08/05/chadema-yaja-na-mfumo-mpya-waliokimbia-watatamani-kurudi/

No comments:

Post a Comment