Monday, August 3, 2020

Nyalandu ampongeza Lissu kuibuka kidedea kugombea Urais

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Kati , Lazaro Nyalandu, amempongeza Tundu Lissu, kwa kupata ushindi mkubwa wa kugombea urais.

Nyalandu ambaye ni miongoni kwa waliochukua fomu ya kugombea urais katika uchaguzi uliofanyika jana alipata kura 36 huku Lissu akiwa amepata kura 405.

“Pongezi sana kaka mh. Tundu Lissu kwa ushindi wa kishindo ulipupata baraza kuu Chadematz kuwa mgombea urais kupitia chama chetu,” aliandika Nyalandu katika ukurasa wake wa Twitter.

Aliongezea ” Nakupongeza kwa dhati na tutashirikiana kuhakikisha Chama Chetu kinashinda,”



source http://www.bongoleo.com/2020/08/04/nyalandu-ampongeza-lissu-kuibuka-kidedea-kugombea-urais/

No comments:

Post a Comment