Monday, August 3, 2020

Cristiano Ronaldo Ajizawidi Gari la TSh 24 Bilioni, Bugatti Centodieci

Stat Attack: Cristiano Ronaldo Has Actually Been Brilliant for ...

Nyota huyo wa kandanda atakuwa kati ya matajiri 10 duniani wanaomiliki gari aina hiyo. Picha: Hisani

Cristiano alivunja rekodi nyingine baada ya kuibuka mshindi Juventus

Nyota huyo alisherehekea ushindi huo kwa gari la kifahari lenye thamani ya TSh 24 bilioni

Ronaldo atakuwa kati ya matajiri 10 wanaomiliki gari hilo duniani

Cristiano Ronaldo ni kati ya wanakandanda tajiri zadi ulimwenguni, kando na utajiri, makali yake ya kandanda si mjadala tena.

Nyota huyo wa kandanda ambaye ametua mataji kadha wa kadha, alivunja rekodi nyingine hivi majuzi akiwa katika klabu ya Juventus.

View this post on Instagram

One more! 🏆 It’s not a bad habit 😉

A post shared by Cristiano Ronaldo (@cristiano) on

Wiki chache baadaye, Ronaldo ameamua kusherekea ushindi wake kwa kujizawidi gari la kifahari la TSh 24 bilioni (£8.5m) Bugatti Centodieci.

Kulingana na jarida laTuttosport, nyota huyo mwenye umri wa miaka 35 alikuwa amemaliza kulipa rasmi  hela za gari hilo na kuahidiwa kukabidhiwa gari hilo 2021.

Gari hilo ambalo ni la lita nane, injini ya W16 pia lina uwezo wa kasi ya maili 236/h.

$8.9M Bugatti Centodieci is Chiron's tribute to EB110 and you can ...

Ronaldo alisherehekea ushindi huo kwa gari la kifahari lenye thamani ya TSh 24 bilioni. Picha; Hisani

Ronaldo amelinunua gari hilo kuchukua nafasi ya gari lake aina ya Bugatti Chiron aliyolinunua kwa TSh8,400 milioni (£2.15m).

Nyota huyo wa kandanda atakuwa kati ya matajiri 10 duniani wanaomiliki gari aina hiyo.



source http://www.bongoleo.com/2020/08/03/cristiano-ronaldo-ajizawidi-gari-la-tsh-24-bilioni-bugatti-centodieci/

No comments:

Post a Comment