Baraza Kuu la Chadema limempitisha aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho,Tundu Lissu, kuwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tundu Lissu amepata kura 405 kati ya kura 442 zilizopigwa sawa na asilimia 91.6
Tundu Lissu atathibitishwa na mkutano mkuu wa Chadema ambao unatarajia kufanyika kesho Agosti 4, 2020.
Lazaro Nyalandu amepata kura 36, huku Mayrose Majinge amepata kura Moja.
source http://www.bongoleo.com/2020/08/03/lissu-apitishwa-kugombea-urais-apata-kura-405/
No comments:
Post a Comment