Monday, August 3, 2020

Yanga Wangangania Morrison Watema 14


Klabu ya Yanga imeweka hadharani majina ya wachezaji 14 waliachwa na timu hiyo baada ya kumalizika kwa mikataba yao pamoja na wanaozungumza nao ili kusitisha mikataba na klabu hiyo.

Wachezaji ambao wameachwa huru baada ya mikataba kuisha ni pamoja na Mrisho Ngassa, David Molinga, Jafary Mohammed, Tariq Seif, Andrew Vicent, Nahodha Papy Kabamba Tshishimbi, Mohammed Issa ‘Banka

Wachezaji ambao Klabu inazungumza nao ili kusitisha mikataba yao ni Ali Mtoni, Muharami Issa Maundu, Ali Ali, Yikpe Gislain, Patrick Sibomana, Eric Kabamba na Rafael Daud.

Wachezaji ambao wanabaki kuendelea kuitumikia timu ya Wananchi ni Farouk Shikhalo, Ramadhan Kabwili, Metacha Mnata, Haruna Niyonzima, Lamine Moro na Bernard Morrison.

Wengine ni Feisal Salum, Juma Mahadhi, Adeyum Saleh, Said Juma Makapu, Balama Mapinduzi, Deus Kaseke, Ditram Nchimbi, Abdullaziz Makame na Paul Godfrey.

Aidha Klabu inaendelea na mazungumzo na wachezaji wake wakongwe, Juma Abdul na Kelvin Yondani ambao mikataba yao imeisha ili kuendelea kuitumikia timu ya Wananchi.



source http://www.bongoleo.com/2020/08/03/yanga-wangangania-morrison-watema-14/

No comments:

Post a Comment