Monday, August 3, 2020

Muuguzi Aliyejifungua Kwenye ICU Aangamizwa na COVID19

Marian Awuor: Homa Bay nurse who gave birth in ICU succumbs to COVID-19

Marian Awuor alijifungua Ijumaa, Julai 24 akiwa ICU baada ya kupatikana na corona

Licha ya kuonyesha dalili za corona, alipimwa virusi hivyo katika hospitali ya Homabay bila kupatikana na virusi

Alihamishwa hadi hospitali ya rufaa ya Kisii alikopimwa na kupatikana na virusi hivyo

Muuguzi katika hospitali ya Homabay aliyejifungua mtoto wa kiume akiwa katika ICU baada ya kupatikana na virusi vya COVID19 amefariki.

Mariam Awuor alihamishwa kutoka katika hospitali ya Homabay hadi hospitali ya rufaa ya Kisii baada ya hali yake kuwa mbaya zaidi na kulazimika kuwekwa katika ICU.

Baada ya kufanyiwa vipimo, alithibitishwa kuugua virusi vya corona. Licha ya hali yake kuzorota, Mariam aliweza kujifungua mtoto wa kiume hospitalini humo kabla kuangamia siku mbili baadaye.

Kwa mujibu wa bodi ya  muungano wa wauguzi nchini, hali ya Mariam ilizorota haswa Jumapili, Agosti 2 na hatimaye kuaga 4pm.

‘’ Mariam alijifungua mtoto wa kiume akipata matibabu.  Aliendelea kupata matibabu akiwa ICU,’’ taarifa hiyo.

Marian Awuor Adumbo, a nurse working at Rachuonyo Sub County Hospital was admitted at Homabay County Hospital with…

Posted by National Nurses Association Of Kenya – NNAK on Sunday, 2 August 2020

Awuor alikuwa muuguzi katika hospitali ya kaunti ndogo ya Rachuonyo, alilazwa katika hospitali ya kaunti ya Homabay ambako alifanyiwa vipimo bila kupatikana na corona.

Hali yake ilipozidi, alihamishwa hadi Kisii alikofanyiwa vipimo vingine na kupatikana na virusi hivo.

Kama ilivyoripotiwa awali na jarida la Bongo Leo, mumewe Mariam aliruhisiwa kumuona mwanawe baada ya kuzaliwa chini ya uangalizi mkali wa madaktari kumuepuka na virusi hivyo.

‘’ Niliandamna na madaktari nikiwa nimevalia magwanda ya kujikinga. Nlimuona mwanangu akiwa kwenye kiangulio,’’ alisema.

Bwana huyo ambaye hakupatikana na virusi vya corona alieleza kuwa walifunga pingu za maisha na Mariam mapema 2019 na walikuwa na hamu kubwa ya kumpokea kifungua mimba wao.



source http://www.bongoleo.com/2020/08/03/muuguzi-aliyejifungua-kwenye-icu-aangamizwa-na-covid19/

No comments:

Post a Comment