Wednesday, August 5, 2020

Zitto: Tutafanya ushirikiano ili kupambana na adui yetu CCM

Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema watafanya ushirikiano ili kupambana na adui yao CCM.

“Nataka kuwahakikishia Watanzania kwamba tutaendelea kufanya juhudi mpaka dakika za mwisho kuhakikisha tunakuwa na mashirikiano ili twende tukapambane na adui yetu CCM tuweze kuibadilisha nchi yetu,” amesema Zitto

Zitto amesema chama cha ACT-Wazalendo ni chama kichanga kuliko vyote vya Tanzania kikiwa na umri wake wa miaka sita tangua kuanzishwa kwake.

Amesema taswira ya mkutano mkuu ni tofauti na uhalisia.



source http://www.bongoleo.com/2020/08/05/zitto-tutafanya-ushirikiano-ili-kupambana-na-adui-yetu-ccm/

No comments:

Post a Comment