Wednesday, August 5, 2020

Rais Magufuli amesema serikali itatoa Sh milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa vibanda vya biashara Dumila

Rais John Magufuli amesema serikali itatoa sh milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa vibanda  kwa ajili ya kufanya shughuli zao za biashara katika eneo la Dumila mkoani Morogoro.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo wakati akitoka Dar es Salaam kuelekea mkoani Dodoma.

Akiwa njiani Rais Magufuli amewasalimia wananchi wa Dumila katika Wilaya ya Mvomero  mkoani Morogoro ambao wanajishughulisha na biashara ndogondogo za kuuza mahindi ya kuchoma, mahindi mabichi, nyanya, vitinguu, mbogamboga na bidhaa nyingine zinazozalishwa katika eneo hilo.

Rais Magufuli amekubali ombi la wananchi hao kupanuliwa kwa barabara na kujengwa kwa vibanda vya biashara katika eneo hilo, kwa kuwa mazingira yalitopo sasa ni finyu na hatarishi kutokana na kusongamana katika barabara kuu.

Rais Magufuli ameahidi kuwa serikali itatoa Sh milioni 100 kwa ajili ha ujenzi wa vibanda hivyo.

Pia Rais Magufuli amemuagiza Meneja wa Wakala wa Barabara (Tanroads) katika mkoa wa Morogoro kufanya upanuzi wa barabara katika eneo hilo.



source http://www.bongoleo.com/2020/08/05/rais-magufuli-amesema-serikali-itatoa-sh-milioni-100-kwa-ajili-ya-ujenzi-wa-vibanda-vya-biashara-dumila/

No comments:

Post a Comment