Sunday, August 2, 2020

Mbowe ampokea Naibu Katibu Mkuu wa Cuf aliyetangaza kujiunga na Chadema

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amempokea Naibu Katiba Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Faki Suleiman Khatib, aliyetangaza kujiunga na chama hicho mbele ya Kamati Kuu jijini Dar es Salaam.

Chadema leo Agosti 02, 2020 kimeanza vikao vya ndani vya chama hicho ambavyo vitahitimishwa kwa kufanya uteuzi wa mgombea wa urais na mgombea mwenza wa Urais.

Wajumbe wa Chadema kutoka mikoa mbalimbali wamefika Dar es Salaam kwa ajili ya kushiriki vikao vya chama ambacho kikao cha kwanza kufanyika ni cha kamati kuu.



source http://www.bongoleo.com/2020/08/02/mbowe-ampokea-naibu-katibu-mkuu-wa-cuf-aliyetangaza-kujiunga-na-chadema/

No comments:

Post a Comment