Saturday, August 1, 2020

DONDOO ZA LEO; Kenya yaomba poo, Marekani yawaumbua, Waziri nje kwa ngono

Habari ya asubuhi mdau wa Opera News, tunatumai u bukheri wa afya.

Karibu katika dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari nchini asubuhi ya leo.

Zinazobamba leo ni pamoja na Marekani kuiorodhesha Tanzania kama nchi salama kwa raia wake kutembelea, Kenya yasalimu amri na mwisho ni juu ya ngono ilivyootesha kibarua cha Waziri. karibu;

TANZANIA NI SALAMA

IDARA ya Ushauri wa Afya ya Marekani imeitaja nchi ya Tanzania kuwa ni miongoni mwa nchi salama ambazo wananchi wake (Wamarekani) wanaweza kuitembelea katika majira haya ya joto.

Taarifa iliyotolewa na idara hiyo na kutangazwa na kituo cha Televisheni cha CNN, imesema wananchi wake wanaweza kuitembelea Tanzania lakini wakifika lazima wafanye vipimo vya Covid-19 kabla ya kuendelea na shughuli zao.

Soma zaidi>>>

KENYA YAUFYATA

Saa chache baada ya Tanzania kuzuia ndege za Shirika la Ndege la Kenya kuingia nchini, serikali ya Kenya imesema kuwa haijazuia ndege za Tanzania kuingia nchini humo.

Akizungumza katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) jijini Nairobi, Waziri wa Uchukuzi nchini humo James Macharia amesema kilochofanyika ni kuwekwa taratibu za kudhibiti virusi vya corona kwa wageni watakaofika Kenya.

“Hatujapiga marufuku nchi yoyote kuingia Kenya. Hatujafunga anga letu, kile tulichofanya ni kuweka utaratibu wa karantini kwa baadhi ya nchi kulingana na tathmini ya janga hilo,” amesema Macharia.

Waziri huyo amesema tayari wamefanya mazungumzo na Tanzania na wamemaliza sintofahamu iliyokuwepo na kabla ya siku kumalizika wananchi wa pande hizo mbili wataruhusiwa kutoka na kuingia katika nchi hizo.

NGONO YAMPONZA WAZIRI

RAIS  wa Zambia, Edgar Lungu, amemfukuza kazi Waziri wa Elimu nchini humo, David Mabumba, baada ya kuvuja kwa video ya ngono inayomuonyesha Mabumba ambaye yupo karantini akijamiiana na mwanamke kwa njia ya simu (video call), inadaiwa kuwa mwanamke huyo ni mke wa mtu.

Soma zaidi>>>

 

 



source http://www.bongoleo.com/2020/08/02/kenya-yaomba-poo-marekani-tanzania-ni-salama-nendeni-waziri-nje-kwa-ngono/

No comments:

Post a Comment