Wednesday, August 5, 2020

COVID19: India Yarekodi vifo 857, Maambukizi 52,509 Chini ya saa 24

India coronavirus, COVID-19 live updates, May 17: Maharashtra's ...

Jumanne, Agosti 4, India ilirekodi zaidi ya vifo 857 kutokana na virusi hivyo. Picha; Hisani.

India ina jumla ya visa vya maambukizi 19,08,254 ya covid19

Hadi sasa, zaidi ya vifo  39,797 vimetangazwa na wizara ya afya

Jumanne, Agosti 4, India ilirekodi zaidi ya vifo 857 kutokana na virusi hivyo

Huku virusi vya corona vikizidi kushambulia kila eneo duniani, kila taifa linazidi kujizatiti kutafuta suluhu la kudumu katika kujikinga na kuzuia madhara zaidi kutokana na virusi hivyo.

Hata baada ya Rais Pombe Magufuli kutangaza kuwa Tanzania imepiga teke virusi hivyo kutona na neema ya Mungu, nchi majirani na zile za mbali zimezidi kuangamizwa na virusi hivyo.

Covid-19 LIVE updates: India has 29,974 cases; Centre says no ...

Kulingana na jarida la Tribune, nchi ya India iliweza kurekodi zaidi ya vifo  857 pamoja na maambukizi 52,509 chini ya saa 24 Jumanne, Agosti 4. Hii ni baada ya takriban watu 619, 652 kufanyiwa vipimo

Kwa mujibu wa wizara ya afya ya nchi hiyo, India ni mojawapo ya nchi ambayo imeweza kudhibiti virusi vya corona kwa kiwango kikubwa, idadi ya wanaopona kutokana na virusi hivyo ikiwa ni 67.19% huku wanaofariki wakiwa 2.08%.

Aidha, eneo la Maharashtra ndilo limekuwa ngome ya ya virusi vya covid19 nchini humo idadi ya maambukizi ikifika 450,196  pamoja na vifo 15,842.



source http://www.bongoleo.com/2020/08/05/covid19-india-yarekodi-vifo-857-maambukizi-52509-chini-ya-saa-24/

No comments:

Post a Comment